• HABARI MPYA

    Saturday, February 24, 2024

    FODEN AING’ARISHA MAN CITY YAICHAPA BOURNEMOUTH 1-0 VITALITY


    BAO pekee la kiungo Muingereza, Philip Walter Foden dakika ya 24 limeipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vitality, Bournemouth, Dorset.
    Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 59, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Liverpool baada wote kucheza mechi 26, wakati Bournemouth inabaki na pointi 28 za mechi 25 nafasi ya 14.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FODEN AING’ARISHA MAN CITY YAICHAPA BOURNEMOUTH 1-0 VITALITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top