• HABARI MPYA

  Thursday, February 01, 2024

  LIVERPOOL YAITANDIKA CHELSEA 4-1 NA KUZIDI KUUKARIBIA UBINGWA ENGLAND


  WENYEJI, Liverpool usiku wa jana wameitandika Chelsea mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Diogo Jota dakika ya 23, Conor Bradley dakika ya 39, Dominik Szoboszlai dakika ya 65 na Luis Díaz dakika ya 79, wakati la Chelsea lilifungwa na Christopher Nkunku dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 51 katika mchezo wa 22 na kuendelea kuongoza Ligi mbele ya mabingwa watetezi, Manchester City wenye pointi 46 za mechi 21, wakati Chelsea inabaki na pointi zake 31 za mechi 22 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAITANDIKA CHELSEA 4-1 NA KUZIDI KUUKARIBIA UBINGWA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top