• HABARI MPYA

  Thursday, February 29, 2024

  IHEFU SC YABANWA NYUMBANI, YATOA SARE NA MSHUJAA 1-1

  WENYEJI, Ihefu SC jana wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja LITI mjini Singida.
  Mshambuliaji Mkenya, Elvis Rupia alianza kuifungia Ihefu SC dakika ya 11, kabla ya Omary Omary kuisawazishia Mashujaa dakika ya 73.
  Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi 20, japokuwa inabaki nafasi ya 11 na Mashujaa inatimiza pointi 15, ingawa inabaki nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 18. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YABANWA NYUMBANI, YATOA SARE NA MSHUJAA 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top