• HABARI MPYA

  Monday, February 19, 2024

  WASHINDI WA MTOKO WA KIBINGWA 56 KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO


  KAMPUNI namba moja ya michezo ya kubashiri nchini Betika imezindua rasmi Kampeni yake kubwa ya "Mtoko wa Kibingwa " kwa Msimu wa 7 kwa wateja wake na kuendelea kutimiza ndoto za mashabiki wa  soka.

  Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 19,2024 Afisa Habari wa Betika Rugambwa Juvenalius amesema Kampeni hiyo imezinduliwa Leo ambapo droo zitaanza Februari 27,2024 hadi kufikia tamati Aprili 10,2024 na Mabingwa 56 kushuhudia derby ya watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga katika Jukwaa la VIP A. 
  Aidha Juvenalius ameeleza sababu ya kuwepo kwa Kampeni hiyo ina lenga kuwaleta pamoja mashabiki wa soka na kuwapa fursa ya kufurahia burudani ya kipekee ya kushuhudia mechi ya watani wa jadi bila longolongo.
  "Kampuni yetu ya Betika katika mtoko huu wa Kibingwa itahakikisha inatoq zawadi za wiki,za mwezi pamoja na Usafiri wa Tiketi za Ndege kwa washindi watakaopatikana Mikoani na gharama za kila kitu zitalipwa na sisi wenyewe betika ."


  Pia amesema kampeni hiyo inamuhitaji mshiriki abashiri kwa mikeka mitatu ambapo dau lake ni shilingi elfu 2 tu.
  "Mshiriki atatakiwa kuweka ubashiri kwa dau la 2,000 mechi zaidi ya 3 anaingia kwenye droo ya ushindi ".
  "Hata hivyo watakaobashiri mara nyingi zaidi kwa wiki na kutofanikiwa kushinda mikeka hiyo watapata zawadi ya simu Android wakati watakaobashiri zaidi kwa mwezi watajishindia simu aina ya Iphone 15.
  "Kumbuka mkeka utiki au usitiki unaingia kwenye droo ya kushinda mtoko wa kibingwa hivyo waendelee kuweka ubashiri wao kupitia www.betika.co.tz au piga *149*16#..
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WASHINDI WA MTOKO WA KIBINGWA 56 KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top