• HABARI MPYA

  Friday, February 23, 2024

  TWIGA STARS YALAMBEA 3-0 NA BANYANA BANYANA CHAMAZI


  TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imechapwa mabao 3-9 na Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza Raundi ya Tatu kufuzu Olimpiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Banyana Banyana yamefungwa na Jermaine Seoposenwe dakika ya 10, Thembi Kgatlana dakika ya 57 na Hilda Magaia dakika ya 85.
  Timu hizo zirudiana Februari 27 Uwanja wa Mbombela, Nelspruit nchini Afrika Kusini na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla katí ya Cameroon na Nigeria kuwania tiketi moja kati ya mbili za Afrika kwenye Olimpiki ya Paris inayotarajiwa kuanza Julai 24 hadi Agosti 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YALAMBEA 3-0 NA BANYANA BANYANA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top