• HABARI MPYA

  Tuesday, February 20, 2024

  TIMU ZA LIGI KUU ZAZICHUJA ZA CHAMPIONSHIP KWENYE ASFC


  TIMU za Coastal Union, Singida Fountain Gate na Dodoma Jiji zimelinda hadhi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuzitoa timu za NBC Championship katika Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
  Coastal Union iliichapa Mbeya Kwanza 1-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, Singida Fountain Gate ikaichapa 2-0 Fountain Gate Talents Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza na Dodoma Jiji ikailaza 2-1 Biashara United Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Michuano ya ASFC Hatua ya 32 Bora inaendelea leo kwa mabingwa watetezi, Yanga kumenyana na Polisi Tanzania kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  FEBRARI 20, 2024
  Mashujaa FC         v Mkwajuni
  KMC v Gunners FC
  Yanga SC v Polisi Tanzania
  Kagera Sugar         v Pamba FC
  FEBRUARI 21, 2024
  Mtibwa Sugar         v Stand nited
  Namungo FC         v Transit Camp
  FEBRUARI 22, 2024
  Tabora United         v Nyamongo SC
  Azam FC v Green Warriors
  Ihefu SC         v Mbuni FC
  JKT Tanzania         v TMA Stars
  Geita Gold         v Mbeya City
  FEBRUARI 27, 2024
  Simba SC v TRA Kilimanjaro

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU ZA LIGI KUU ZAZICHUJA ZA CHAMPIONSHIP KWENYE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top