• HABARI MPYA

  Thursday, February 01, 2024

  MANCHESTER CITY YAICHAPA BURNLEY 3-1 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City usiku wa jana wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Julian Álvarez mawili, dakika ya 16 na 22 na Rodri dakika ya 46, wakati la Burnley limefungwa na A. Al Dakhil dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 21 na kurejea nafasi ya pili, nyuma ya Liverpool inayoongoza kwa pointi zake 51 za mechi 22, wakati Arsenal yenye pointi 46 za mechi 22 ni ya tatu.
  Kwa upande wao Burnley baada ya kichapo cha jana inabaki na pointi zake 12 za mechi 22 nafasi ya 19 kwenye Ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAICHAPA BURNLEY 3-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top