• HABARI MPYA

  Monday, February 12, 2024

  IHEFU YAWACHAPA MTIBWA SUGAR 3-2 PALE PALE MANUNGU


  TIMU ya Ihefu SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Ihefu SC yamefungwa na viungo, Mkenya Duke Abuya dakika ya 15, Mtogo Marouf Tchakei dakika ya 29 na mshambuliaji Mkenya Elvis Rupia dakika ya 73, wakati ya Mtibwa Sugar yamefungwa na kiungo Kassim Shabani Haruna dakika ya 42 mshambuliaji Juma Luizio Ndanda dakika ya 46.
  Kwa ushindi huo, Ihefu SC wanafikisha pointi 16 na kusogea nafasi ya 12, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake nane na kuendelea kushika mkia baada ya wote kucheza mechi 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU YAWACHAPA MTIBWA SUGAR 3-2 PALE PALE MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top