• HABARI MPYA

  Thursday, February 15, 2024

  TANZANIA PRISONS YAITANDIKA SINGIDA FOUNTAIN GATE 3-1 SOKOINE


  WENYEJI, Tanzania Prisons wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Tanzania Prisons yamefungwa na Zabona Mayombya, mawili dakika ya 15 na 73 na Sansón Mbangula dakika ya 59, wakati bao pekee la Singida Fountain Gate limefungwa na Bruno Gomes dakika ya 27.
  Tanzania Prisons wanafikisha pointi 20 na kupanda nafasi ya sita, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi 20 na inashukia nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA PRISONS YAITANDIKA SINGIDA FOUNTAIN GATE 3-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top