• HABARI MPYA

  Monday, February 19, 2024

  HOJLUND APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA LUTON 2-1


  TIMU ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Luton Town katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Kenilworth Road mjini Luton, Bedfordshire.
  Mabao yote ya Manchester United yalifungwa na mshambuliaji chipukizi wa Kimataifa wa Denmark, Rasmus Winther Hojlund (21) dakika ya kwanza na ya saba alísela rekodi ya mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufunga katika mechi sita mfululizo za Ligi Kuu ya England 
  Bao pekee la Luton Town limefungwa na mshambuliaji Carlton John Morris dakika ya 14 na kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 44, ingawa wanabaki nafasi ya sita wakizidiwa pointi tatu na Tottenham Hotspur baada ya wote kucheza mechi 25.
  Luton Town wao baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 20 za mechi 24 nafasi ya 17 kwenye Ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka Daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HOJLUND APIGA MBILI MAN UNITED YAICHAPA LUTON 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top