• HABARI MPYA

  Saturday, February 03, 2024

  SERENGETI BOYS WAFUNGWA 5-0 NA MABINTI WA KIZAMBIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imefungwa mabao 5-0 na wenyeji, Zambia katika mchezo wa kwanza Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia leo Uwanja wa Nkoloma Jijini Lusaka.
  Mabao ya Zambia yamefungwa na Saliya Mwanza dakika ya 29, Zangose Zulu dakika ya 31 na 45 na ushei, Chileshe Bwalya dakika ya 77 na Ruth Muwowo dakika ya 90 na ushei.
  Timu hizo zitarudiana Jumapili ya Februari 11 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Uganda na Cameroon katika Raund ya Tatu.
  Kutakuwa na Raundi ya Nne na ya mwisho na washindi watatu ndiyo wataiwakilisha Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambazo zitafanyika Jamhuri ya Dominican.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS WAFUNGWA 5-0 NA MABINTI WA KIZAMBIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top