• HABARI MPYA

    Monday, February 19, 2024

    BENCHIKA ATEUA 22 KUIFUATA ASEC KWA MECHI YA IJUMAA


    KOCHA Mualgeria, Abdelhak Benchika ameteua wachezaji 22 kwa safari ya Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa Kundi B Ligi ya Mbingwa Afrika dhidi ya wenyeji, ASEC Mimosas Ijumaa.
    Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny Jijini Abidjan utaanza Saa 4:00 usiku kwa Saa za Tanzania.
    Kuelekea mechi mbili za mwisho, Simba SC inashika nafasi ya pili Kundi B ikiwa na pointi tano, nyuma ya ASEC Mimosas yenye pointi 10 na mbele ya Jwaneng Galaxy ya Botswana yenye pointi nne na Wydad Athletic ya Morocco yenye pointi tatu baada ya wote kucheza mechi nne.
    Wakati ASEC wakiwa wenyeji wa Simba wikiendi hii, Wydad watakuwa wageni wa Jwaneng Galaxy huko Botswana.
    Mechi za mwisho ni Simba na Jwaneng Galaxy Jijini Dar es Salaam na Wydad dhidi ya ASEC Jijini Casablanca.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENCHIKA ATEUA 22 KUIFUATA ASEC KWA MECHI YA IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top