• HABARI MPYA

  Friday, February 16, 2024

  AZAM FC YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na mawinga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 44 na mzawa, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 85, wakati bao pekee la Geita Gold limefungwa na mshambuliaji mzawa, Tariq Seif Kiakala dakika ya 41.
  Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi 35, ingawa wanabaki nafasi ya tatu, nyuma ya Simba yenye pointi 36 na Yanga 40 baada ya wote kucheza mechi 15.
  Kwa upande wao Geita Gold baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 16 za mechi 15 pia nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top