• HABARI MPYA

  Saturday, February 17, 2024

  MAKAMU MWENYEKITI SIMBA YA FAINALI CAF 1993 AFARIKI DUNIA


  ALIYEWAHI kuwa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC miaka ya 1990, Fakhruddin Amijee amefariki dunia jana jioni nyumbani kwake Arusha akiwa ana umri wa miaka 84 baada ya kuusmbuliwa na maradhi kwa muda mdupi .
  Amijee aliyewahi pia kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Dar es Salaam (TAREVA) na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Tanzania (TABA) amezikwa jana hiyo hiyo usiku Jijini Arusha.
  Amijee alikuwa Makamu Mwenyekiti Simba kuanzia mwaka 1990 chini Mikidadi Kasanda, Juma Salum baadaye chini ya Ally Amir ‘Bamchawi’ na Priva Mtema (wote marehemu) mwaka 1996 na baada ya hapo akahamia kwenye michezo mingine na kuongoza TAVA na TABA.


  Enzi za uhai wake marehemu Amijee alikuwa kiongozi wa msafara wa mechi zote za ugenini Simba wakifika Fainali Kombe la CAF mwaka 1993.
  Lakini pia atakumbukwa kwa kuileta klabu ya Stoke City ya England ambayo ilicheza mechi za kirafiki na timu za Simba, Yanga Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Coastal Unión Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Amijee ameacha mke, Sukaina na watoto watatu, Zahra, Husain na Zainab.
  Mungu ampumzishe kwa amani. Amín. 


  Kipa wa Yanga SC, Stephen Nemes (kulia) akinyoosha mguu dhidi ya Ernie Tapei wa Stoke City ya England  ambayo ililetwa nchini na marehemu Fakhruddin Amijee mwaka 1991.
  Yanga ilifungwa 2-1 Uwanja wa Taifa (Uhuru), Dar es Salaam mwaka 1991
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAKAMU MWENYEKITI SIMBA YA FAINALI CAF 1993 AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top