• HABARI MPYA

  Saturday, February 24, 2024

  KMC YATOA SARE 2-2 NA NAMUNGO FC CHAMAZI


  TIMU za KMC na Namungo FC zimegawana pointi baada ya sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya KMC yamefungwa na Rahim Shomari dakika ya nne na Daruwesh Saliboko dakika ya 50, wakati ya Namungo FC yamefungwa na Meddie Kagere dakika ya 57 na Ibrahim Mkoko dakika ya 61.
  Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 23, ingawa inabaki nafasi ya tano na Namungo FC inafikisha pointi 20, nayo inabaki nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YATOA SARE 2-2 NA NAMUNGO FC CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top