// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MUDATHIR TENA BAO LA JIONIIII…YANGA YAICHAPA MASHUJAA 2-1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MUDATHIR TENA BAO LA JIONIIII…YANGA YAICHAPA MASHUJAA 2-1 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Thursday, February 08, 2024

  MUDATHIR TENA BAO LA JIONIIII…YANGA YAICHAPA MASHUJAA 2-1


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamejiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa FC ya Kigoma leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Winga Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli alianza kuifungia Yanga dakika ya 44 baada ya kazi nzuri ya mshambuliaji Clement Francis Mzize, lakini mshambuliaji Emmanuel Mtumbuka kuisawazishia Mashujaa dakika ya 65 kwa shuti la mbali lililomshinda kipa Abdultwalib Mshery.
  Kwa mara ya pili mfululizo leo shujaa wa Yanga amekuwa kiungo Mudathir Yahya Abbas ‘Zanzíbar Greatest’ aliyefunga bao la ushindi dakika ya 85 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mzambia, Kennedy Musonda.
  Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 37 katika mchezo wa 14 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu mbele ya Azam FC yenye pointi 31 za mechi 13 na Simba SC yenye pointi 29 za mechi 12.
  Mashujaa kwa upande wao hali inazidi kuwa mbaya baada ya kichapo cha leo ikibaki na pointi zake tisa za mechi 14 nafasi ya 15 kwenye Ligi ya timu 16 ambayo mwishowe mbili zitashuka Daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUDATHIR TENA BAO LA JIONIIII…YANGA YAICHAPA MASHUJAA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top