• HABARI MPYA

  Tuesday, February 20, 2024

  GUEDE APIGA MBILI YANGA YAICHAPA POLISI 5-0


  MABINGWA watetezi, Yanga wamefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Polisi Tanzania leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji mpya, Muivory Coast, Joseph Guede, mawili dakika ya 13 na 45 na ushei, wazawa, kiungo Farid Mussa dakika ya 33, mshambuliaji Clement Mzize dakika ya 82 na kiungo mwingine, Sheikhan Ibrahim dakika ya 87 kwa penalti.
  Mechi nyingine ya leo Hatua ya 16 Bora ASFC, KMC imeichapa Gunners 4-0 hapo hapo Azam Complex mabao ya Redemtus Mussa dakika ya tatu, Deogratius Kulwa dakika ya 32, Rashid Chambo dakika ya 79 na Hance Masoud dakika ya 90 na ushei.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GUEDE APIGA MBILI YANGA YAICHAPA POLISI 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top