// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA AZAM FC 1-1 KIRUMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA AZAM FC 1-1 KIRUMBA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Friday, February 09, 2024

  SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA AZAM FC 1-1 KIRUMBA


  IKITUMIA Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kama wa nyumbani, Simba SC leo imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
  Azam FC walitangulia kwa bao la mshambuliaji mzoefu wa kuzifunga Simba na Yanga, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 14 akimalizia pasi ya Paschal Msindo baada ya shambulizi lililoanzishwa na Yahya Zayd.
  Lakini kiungo mshambuliaji Mzambia, Clatous Chotta Chama akaisawazishia Simba SC dakika ya 90 kwa shuti la moja kwa moja la mpira wa adhabu lililomshinda kipa Msudan, Mohamed Mustafa.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 32, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 14, wakati Simba inafikisha pointi 30 katika mchezo wa 13 na inabaki nafasi ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAMBULIA SARE KWA AZAM FC 1-1 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top