• HABARI MPYA

  Tuesday, February 06, 2024

  SIMBA SC YATOA ONYO, YAITANDIKA TABORA 4-0 MWINYI


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Mgambia Pa Omar Jobe dakika ya 20, kiungo wa Mali, Sadio Kanouté dakika ya 36, beki Mcameroon,  Che Fondoh Malone Junior dakika ya 60 na mshambuliaji Muivory Coast, Freddy Michael Kouablan dakika ya 87.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 12, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 34 na Azam FC pointi 31 baada ya wote kucheza mechi 13.
  Kwa upande wao Tabora United wanabaki na pointi zao 15 za mechi 14 nafasi ya 12 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwishowe tatu zitashuka Daraja na mbili zitamenyana zenyewe ili moja ibaki Ligi Kuu.
  Itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu ya Ligi ya Championship kuwania kurudi Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATOA ONYO, YAITANDIKA TABORA 4-0 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top