• HABARI MPYA

  Tuesday, February 13, 2024

  KAGERA SUGAR YAICHAPA SINGIDA 1-0, KMC NA COASTAL 0-0


  BAO pekee la beki David Luhende dakika ya 20 jana liliipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar wanafikisha pointi 17 na kusogea nafasi ya 10, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi zake 20 nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 15.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu jana KMC ilitoa sare ya bila mabao na Coastal Unión Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo KMC inafikisha pointi 22, ingawa inabaki nafasi ya nne na Coastal Unión inafikisha pointi 20, nayo inabaki nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA SINGIDA 1-0, KMC NA COASTAL 0-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top