• HABARI MPYA

  Monday, February 19, 2024

  IHEFU YAWAKANDA GEITA GOLD 2-1 PALE PALE NYANKUMBU


  TIMU ya Ihefu SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Ihefu SC yamefungwa na mshambuliaji Mkenya, Elvis Rupia dakika ya sita na kiungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya 12, wakati bao pekee la Geita Gold limefungwa na Tariq Seif dakika ya 49.
  Kwa ushindi huo, Ihefu SC inafikisha pointi 19 na kusogea nafasi ya 10, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 16 na inashuka kwa nafasi moja hadi ya 14 baada ya wote kucheza mechi sita 16 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU YAWAKANDA GEITA GOLD 2-1 PALE PALE NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top