• HABARI MPYA

  Saturday, February 10, 2024

  MWENYEKITI WA ZAMANI WA YANGA MADEGA AFARIKI WAKILI DUNIA


  ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC, Wakili Imani Omar Mahugila Madega amefariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya Msoga iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Chalinze mkoani Pwani.
  Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Bakari Madega 'Beka Rangers', Wakili Madega amefariki baada ya kusumbuliwa na shinikizo la damu.
  Pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Yanga, kuanzia Mei 30, mwaka 2007 hadi Julai 18 mwaka 2010, Wakili Madega pia amewahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwenyekiti wa Chama Soka Pwani (COREFA) na Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF.
  Mwili wa Wakili Imani Omar Mahugila Madega unatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake, Chalinze mkoani Pwani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWENYEKITI WA ZAMANI WA YANGA MADEGA AFARIKI WAKILI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top