• HABARI MPYA

  Monday, February 19, 2024

  AZAM FC YAAMBULIA SARE KWA TABORA UNITED, 0-0 MWINYI


  TIMU ya Azam FC imetoa sare ya bila mabao na wenyeji, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
  Kwa sare hiyo, Azam FC inafikisha pointi 36 katika mchezo wa 16 na kusogea nafasi ya pili, ikiizidi tu wastani wa mabao Simba SC ambayo pia ina mechi moja mkononi na wote wapo nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 43 za mechi 16.
  Kwa upande wao Tabora United baada ya sare hiyo wanabaki na pointi zao 17 za mechi 16 nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAAMBULIA SARE KWA TABORA UNITED, 0-0 MWINYI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top