• HABARI MPYA

  Wednesday, February 28, 2024

  KIPRE JUNIOR AIBEBESHA AZAM FC POINTI TATU MUHIMU


  BAO pekee la winga Muivory Coast, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon dakika ya 53 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Singida Fountain Gate leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 40 katika mchezo wa 18, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao, Singida Fountain Gate baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 21 za mechi 18 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPRE JUNIOR AIBEBESHA AZAM FC POINTI TATU MUHIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top