• HABARI MPYA

  Saturday, February 24, 2024

  SIMBA SC NA ASEC ZATOSHANA MBAVU ABIDJAN


  TIMU ya Simba SC imetoa sare ya bila mabao na wenyeji, ASEC Mimosas usiku wa Ijumaa katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mbingwa Afrika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny Jijini Abidjan, Ivory Coast.
  Kwa matokeo hayo, Simba SC inayofundishwa na Kocha Mualgeria, Abdelhak Benchika inafikisha pointi sita na inabaki nafasi ya pili, nyuma ya ASEC Mimosas yenye pointi 11 baada ya wote kucheza mechi tano.
  Jwaneng Galaxy ya Botswana yenye pointi nne inashika nafasi ya tatu na Wydad Athletic ya Morocco yenye pointi tatu inashika mkia baada ya wote kucheza mechi nne kuelekea mechi baina yao Jumamosi Botswana.
  Mechi za mwisho ni Simba na Jwaneng Galaxy Jijini Dar es Salaam na Wydad dhidi ya ASEC Jijini Casablanca.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA ASEC ZATOSHANA MBAVU ABIDJAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top