TIMU za Namungo FC na Mtibwa Sugar zimefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuzitoa timu za Ligi ya NBC Championship.
Mtibwa Sugar imeitupa nje Stand United kwa kuichapa mabao 3-2 Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro na Namungo FC imeichapa Transit Camp mabao 3-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment