• HABARI MPYA

  Monday, February 12, 2024

  BABACAR SARR AFUNGA SIMBA YAICHAPA GEITA GOLD 1-0 KIRUMBA


  BAO la kiungo Msenegal, Babacar Sarr dakika ya 81 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 33 na kupanda nafasi ya pili, ikiizidi pointi moja Azam FC baada ya wote kucheza mechi 14 na wote wapo nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 40 za mechi 15.
  Kwa upande wao Geita Gold baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 16 za mechi 14 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BABACAR SARR AFUNGA SIMBA YAICHAPA GEITA GOLD 1-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top