• HABARI MPYA

  Saturday, February 03, 2024

  AZAM FC YAICHAPA MAFUNZO 3-0 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI


  TIMU ya Azam FC leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mafunzo FC ya Zanzibar katika mchezo wa kirafiki inashuka Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC katika mchezo huo wa kujiandaa na mechi zake zijazo za Ligi Kuu, ikiwemo dhidi ya Simba SC Februari 9 yamefungwa na kiungo Adolph Mtasigwa, winga Abdul Suleiman Sopu na beki Baraka Abdallah aliyejifunga.
  Ikumbukwe Jumatano Azam FC walicheza mechi ya kirafiki na timu nyingine ya Zanzibar, KVZ hapo hapo Azam Complex, Chamazi na kuibuka na ushindi wa 3-1, mabao yao yakifungwa na Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo na Wasenegal, Alassane Diao na beki Cheikh Sidibe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA MAFUNZO 3-0 MECHI YA KIRAFIKI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top