• HABARI MPYA

  Thursday, February 15, 2024

  CHAMA KATIKA UBORA WAKE, SIMBA YAICHAPA JKT 1-0 MBWENI


  BAO pekee la kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama dakika ya 33 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, JKT Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 36, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 15, wakati JKT Tanzania inabaki na pointi zake 16 za mechi 15 na inashuka kwa nafasi moja hadi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA KATIKA UBORA WAKE, SIMBA YAICHAPA JKT 1-0 MBWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top