• HABARI MPYA

  Saturday, February 03, 2024

  NIGERIA NA DRC ZATINGA NUSU FAINALI AFCON KWA KUZITOA ANGOLA NA GUINEA


  TIMU za Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana zilifanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Ivory Coast baada ya ushindi dhidi ya Angola na Guinea katika michezo ya Robo Fainali. 
  Walianza Nigeria kuitupa nje Angola kwa kuichapa 1-0 bao pekee la winga wa Atalanta ya Italia, Ademola Lookman Olajade Alade Aylola Lookman dakika ya 41 Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan.
  Baadaye DRC wakatoka nyuma na kuitandika Guinea mabao 3-1 Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara Jijini Abidjan.
  Guinea walitangulia kwa bao la penalti la mshambuliaji wa Le Havre ya Ufaransa, Mohamed Lamine Bayo dakika ya 20, kabla ya DRC kuzinduka kwa mabao ya beki wa Marseille ya Ufaransa, Chancel Mangulu Mbemba dakika ya 27, kiungo wa Brentford ya England, Yoane Wissa Bileko kwa penalti dakika ya 65 na beki wa Besiktas ya Uturuki, Fuka-Arthur Masuaku Kawela dakika ya 82.   
  Sasa Nigeria itakutana na mshindi kati ya Cape Verde na Afrika Kusini na DRC itakutana na mshindi kati ya Mali na Ivory Coast zinazomenyana leo kukamilisha Hatua ya Robo Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIGERIA NA DRC ZATINGA NUSU FAINALI AFCON KWA KUZITOA ANGOLA NA GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top