• HABARI MPYA

  Sunday, January 01, 2023

  CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA NOTTINGHAM FOREST 1-1


  WENYEJI, Nottingham Forest wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground huko Nottingham, Nottinghamshire.
  Chelsea walitangulia kwa bao la Raheem Sterling dakika ya 16, kabla ya Sèrge Aurier kuisawazishia Nottingham Forest dakika ya 63 akimalizia kazi nzuri ya Muivory Coast mwenzake, Willy-Arnaud Zobo Boly.
  Kwa matokeo hayo, Nottingham inafikisha pointi 14 katika mchezo wa 17 nafasi ya 18, wakati Chelsea inafikisha pointi 25 mchezo wa 16 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAAMBULIA SARE KWA NOTTINGHAM FOREST 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top