• HABARI MPYA

  Monday, November 21, 2022

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Ismail Mhesa dakika ya 45 na ushei na Onesmo Mayaya dakika ya 48, wakati la Polisi limefungwa Ambroce Awio dakika ya 35.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya nne, wakati Polisi Tanzania inabaki na pointi zake tisa za mechi 13 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top