• HABARI MPYA

  Tuesday, November 15, 2022

  DODOMA JIJI YAICHAPA KMC 2-1 UHURU


  TIMU ya Dodoma Jiji imeibuka na ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja we Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na mshambuliaji wake tegemeo, Seif Abdallah Karihe dakika ya nane na 18, wakati la KMC alijifunga beki Anderson Solomon dakika ya 48.
  Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji inafikisha pointi tisa katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya 14, wakati KMC inabaki na pointi zake 14 za mechi 12 sasa katika nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA KMC 2-1 UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top