• HABARI MPYA

    Wednesday, November 30, 2022

    CHAMBO AIFUNGIA DODOMA JIJI YAICHAPA COASTAL 1-0


    TIMU ya Dodoma Jiji FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Bao pekee la Dodoma Jiji FC limefungwa na mchezaji wa zamani wa Coastal Union hiyo hiyo, Rashid Chambo dakika ya 90.
    Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya 13, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 12 pia za mechi 13 nafasi ya 12.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHAMBO AIFUNGIA DODOMA JIJI YAICHAPA COASTAL 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top