• HABARI MPYA

  Thursday, November 03, 2022

  MARIOO APEWA UBALOZI WA PARIMATCH


  KAMPUNI ya Mchezo wa ubashiri ya Parimatch  imemtangaza rasmi Msanii wa Bongofleva Omary Ally maarufu kama "Marioo" kuwa balozi wa Kampuni hiyo ili kuwakutanisha mashabiki wake katik michezo ya ubashiri. 
  Akizungumza Leo Novemba 3 Jijini Dar es salaam  Mkurugenzi wa Kampuni ya Parimatch  Erick  Gerald  amesema  ujio wa Marioo umekuwa mzuri kwani kwa sasa Parimatch ndio Kampuni namba moja ya ubashiri ikiwa na ofa za kijanja na tovuti yenye muonekano mzuri,kasi kubwa.
  "Tumechukua hatua ya uthubutu na kumchagua  Marioo kama balozi wetu kwa ajili ya kuzidi kupata burudani hivyo Marioo amepambana na ameweza kufanya vizuri huwezi kuongelea Muziki wa Bongofleva bila kumtaja Marioo."
  Hata hivyo ameeleza namna ubalozi wake utachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza wateja wapya pamoja na kusaidia kutoa uelewa kwa wachezaji hasa ya kubeti ili wote waweze kushinda.
  Kwa upande wake Mwakilishi kutoka bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini  Emmanuel  ndaki amewapongeza Kampuni ya Parimatch kwa kuunganisha tasnia ya muziki kuwa sehemu  ya Michezo ya ubashiri. 
  "Ni hatua kubwa kwa Kampuni ya Parimatch  kuona juhudi za wasanii wa muziki wa Bongofleva  kuingia kwenye Michezo na kuleta hamasa kubwa kuendelea na mchezo wa kubashiri kuongeza pato la taifa na kuhakikisha mchezo huu unakua wa kistaarab.''
  Kwa upande  wake Msanii wa Bongofleva  Omary Ally Mwanga ameshukuru uongozi wa parimatch kumkaribisha kwenye familia yao kwani ni Kampuni ambayo ni kinara wa Michezo ya ubashiri mtandaoni. 
  Marioo mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa balozi wa Kampuni hiyo  kwa muda wa mwaka mmoja ,amesema kutokana na ushawishi wake kwenye tasnia ya muziki ana amini pia ana mashabiki wengine kwenye Michezo ya ubashiri. 
  "Kutangazwa kwangu kuwa balozi naenda kuunganisha mashabiki zangu wa Michezo ya kubashiri na burudani kuwa sehemu moja."
  Hata hivyo Marioo ameeleza namna fursa hiyo ya parimatch inaenda kumkutanisha kwenye michezo ya ubashiri.


  Mkurugenzi wa Kampuni ya ubashiri ya Parimatch  Erick Gerald wakishikana mikono mara baada ya kumalizika kwa utambulisho wa Msanii wa Bongofleva Omary Ally Mwanga maarufu kama  "Marioo" kuwa balozi wa Kampuni ya Parimatch  kwa muda wa mwaka mmoja kama sehemu ya kuongeza wateja wapya wa mchezo wa ubashiri pamoja na kuleta ushindi na siri ya kushinda ubashiri wao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MARIOO APEWA UBALOZI WA PARIMATCH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top