• HABARI MPYA

  Sunday, November 20, 2022

  AZAM FC YAIPIGA NAMUNGO 1-0 MAJALIWA NA KUREJEA KILELENI


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC usiku huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki  Charles Edward Manyama dakika ya 29 akimalizia kazi nzuri ya kiungo, Ayoub Reuben Lyanga.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 13 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi pointi mbili Simba SC ambayo imecheza mechi 12.
  Mabingwa watetezi, Yanga SC sasa wanashukia nafasi ya tatu na pointi zao 26 za mechi 10, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 15 za mechi 12 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA NAMUNGO 1-0 MAJALIWA NA KUREJEA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top