• HABARI MPYA

  Sunday, November 13, 2022

  BRENTFORD YAICHAPA MAN CITY 2-1 PALE PALE ETIHAD


  MABINGWA watetezi, Manchester City jana wamechapwa mabao 2-1 na Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Pongezi kwa mshambuliaji wa England, Ivan Toney aliyeifungia mabao yote Brentford FC dakika ya 19 na 90 na ushei, wakati bao pekee la Man City lilifungwa na Phil Foden dakika ya 45 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Brentford FC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 15 na kusogea nafasi ya 10, wakati Man City inabaki na pointi zake 32 katika nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BRENTFORD YAICHAPA MAN CITY 2-1 PALE PALE ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top