• HABARI MPYA

  Monday, November 07, 2022

  RUVU SHOOTING YATOA SARE 1-1 NA PRISONS UHURU


  TIMU ya Ruvu Shooting imelazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Tanzania Prisons walitangulia na bao la mshambuliaji wake tegemeo, Samson Mbangula dakika ya 49, kabla ya Abalkassim Suleiman kuisawazishia Ruvu Shooting kwa penalti dakika ya 58.
  Kwa matokeo hayo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 11 katika mchezo wa 11 nafasi ya 12, wakati Prisons sasa ina pointi 14 za mechi nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RUVU SHOOTING YATOA SARE 1-1 NA PRISONS UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top