• HABARI MPYA

  Thursday, November 17, 2022

  MBEYA CITY YATOA SARE 2-2 NA KAGERA SUGAR

  WENYEJI, Mbeya City wamelazimishwa sare ya 2-2 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Kagera Sugar walitangulia kwa mabao ya Anuary Jabir dakika ya 18 na Mbaraka Yussuf dakika ya 48, kabla ya Mbeya City kuchomoa kwa mabao ya Tariq Seif dakika ya 61 na Hassan Mahmoud dakika ya 81.
  Kwa sare hiyo, Mbeya, inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya sita, wakati Kagera Sugar imefikisha pointi 12 katika mchezo wa 12 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YATOA SARE 2-2 NA KAGERA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top