• HABARI MPYA

  Sunday, November 06, 2022

  MAN CITY YAIBAMIZA FULHAM 2-1 ETIHAD


  TIMU ya Manchester City imepata ushindi wa 2-1 jana dhidi ya Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad.
  Mabao ya Man City yamefungwa na 
  Julian Alvarez dakika ya 16 na mtokea benchi Erling Haaland kwa penalti dakika ya 90 baada ya Kevin de Bruyne kuangushwa, wakati la Fulham limefungwa na Julian Alvarez kwa penalti pia dakika ya 28 baada ya Joao Cancelo kumchezea rafu Harry Wilson kwenye boksi na kutolewa kwa kadi nyekundu.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 13 na kurejea kileleni wakiizidi Arsenal pointi moja na mechi moja ya kucheza, wakati Fulham inabaki na pointi zake 19 za mechi 14 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIBAMIZA FULHAM 2-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top