• HABARI MPYA

  Thursday, November 17, 2022

  POLISI TANZANIA YAICHAPA IHEFU 2-1 MBARALI

  TIMU ya Polisi Tanzania imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Highland Estate, Mbarali mkoani Mbeya.
  Mabao ya Polisi Tanzania yamefungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 51 na Samuel Onditi aliyejifunga dakika ya 79 baada ya Andrew Simchimba kuanza kuwafungia Ihefu SC kwa penalti dakika ya 19.
  Kwa ushindi huo, Polisi Tanzania inafikisha pointi tisa katika mchezo wa 12, ingawa inabaki nafasi ya 15, wakati Ihefu SC inaendelea kushika mkia kwa pointi zake tano za mechi 11 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YAICHAPA IHEFU 2-1 MBARALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top