• HABARI MPYA

  Wednesday, November 09, 2022

  YANGA YAICHAPA AFRICAIN 1-0 NA KUTINGA MAKUNDI SHIRIKISHO


  KLABU ya Yanga imefanikiwa kwenda Hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Club Africain usiku huu Uwanja wa Olimpiki mjini Rades nchini Morocco.
  Bao pekee la Yanga leo limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 79 kwa shuti akimalizia pasi ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele.
  Yanga wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 1-0 kufuatia sare ya bila kufungana Jumatano iliyopita Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA AFRICAIN 1-0 NA KUTINGA MAKUNDI SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top