• HABARI MPYA

  Wednesday, November 16, 2022

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Adam Adam dakika ya pili na Juma Nyangi dakika ya 32, wakati la Coastal Union limefungwa na Mubarak Hamza dakika ya 23.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya tano, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 12 za mechi 10 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top