• HABARI MPYA

  Sunday, November 13, 2022

  NUNEZ APIGA MBILI LIVERPOOL YASHINDA 3-1  WENYEJI, Liverpool jana wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yalifungwa na Roberto Firmino dakika ya sita na mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay, Darwin Nunez dakika ya 21 na 42, wakati la Southampton lilifungwa na mshambulaji wa kimataifa wa Scotland mzaliwa wa England, Che Zach Adams dakika ya tisa.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 22 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya sita, wakati Southampton inabaki na pointi zake 12 za mechi 15 nafasi ya 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NUNEZ APIGA MBILI LIVERPOOL YASHINDA 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top