• HABARI MPYA

  Saturday, November 26, 2022

  MAYELE APIGA MBILI YANGA YASHINDA 2-0 DAR


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Ilikuwa siku nyingine nzuri kazini kwa mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele aliyefunga mabao yote mawili dakika ya 24 na 49.
  Huo ni mwendelezo wa rekodi ya kutopoteza mechi ya Ligi katika michezo 49 ndani ya misimu mitatu.
  Kwa ushindi huo, Yanga wanafikisha pointi 32 katika mchezo wa 12 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tatu zaidi ya Azam FC wanaofuatia na nne zaidi ya mtani, Simba ambao wote wamecheza mechi 13.
  Mbeya City kwa upande wao baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 19 za mechi 14 nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA MBILI YANGA YASHINDA 2-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top