• HABARI MPYA

  Wednesday, November 09, 2022

  SIMBA QUEENS YATOLEWA KWA KICHAPO CHA 1-0 CHA MAMELODI


  SAFARI ya Simba Queens katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imefikia hatua ya Nusu Fainali baada ya leo kuchapwa bao 1-0 na mabingwa watetezi, Mamelodi Sundown Uwanja wa Prince Moulay EL Hassan mjini Rabat nchini Morocco.
  Bao pekee la Mamelodi Sundown limefungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Lesotho, Boitumelo Joyce Rabale dakika ya 76 akimalizia kazi nzuri ya nyota wa Banyana Banyana, Melinda Kgadiete.
  Nusu Fainali ya pili inafuatia hivi sasa baina ya wenyeji, FAR Rabat na Bayelsa Queens ya Nigeria hapo hapo Uwanja wa Prince Moulay EL Hassan.
  Kwa kuishia Nusu Fainali, Simba Queens itazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani 200,000 wakati bingwa atapata dola 400,000 na mshindi wa pili dola 250,000.
  Timu mbili zilizomaliza nafasi ya tatu katika makundi dola 150,000 kila moja na nyingine mbili zilizoshika mkia dola 100,000 kila moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YATOLEWA KWA KICHAPO CHA 1-0 CHA MAMELODI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top