• HABARI MPYA

  Wednesday, November 23, 2022

  MBEYA CITY YATOA SARE NA SIMBA 1-1 SOKOINE


  WENYEJI, Mbeya City wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Ni Simba SC waliotangulia na bao la kiungo Muzamil Yassin dakika ya 15, kabla ya Tariq Seif kuisawazishia Mbeya City dakika ya 79.
  Kwa matokeo hayo, Simba inafikisha pointi 28 katika mchezo wa 13, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi moja moja na zote, Yanga iliyocheza mechi 11 na Azam FC mechi 13 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YATOA SARE NA SIMBA 1-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top