• HABARI MPYA

  Thursday, November 03, 2022

  CHELSEA YAMALIZA MAKUNDI NA USHINDI WA 2-1


  WENYEJI, Chelsea jana wamehitimisha mechi zao za Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Dinamo Zagreb ya Croatia Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
  Mabao ya Chelsea yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya 18 na Denis Zakaria dakika ya 30, baada ya Dinamo Zagreb kutangulia na bao la Bruno Petković dakika ya saba.
  Kwa ushindi huo, Chelsea inamaliza na pointi 13 mbele ya AC Milan yenye pointi 10, Salzburg pointi sita na Dinamo Zagreb pointi nne.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAMALIZA MAKUNDI NA USHINDI WA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top