• HABARI MPYA

  Friday, November 11, 2022

  GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 KMC NYANKUMBU


  WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Ni Geita Gold waliotangulia na bao la kiungo wake mshambuliaji Mrundi, Said Ntibanzokiza dakika ya 36, kabla ya KMC kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake, Waziri Junior dakika ya 41.
  Kwa matokeo hayo, kila timu inafikisha pointi 14 katika mchezo wa 11, KMC nafasi ya nane Geita Gold nafasi ya 10, zote zikilingana pointi na Tanzania Prisons iliyocheza mechi 11 oí nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 KMC NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top