• HABARI MPYA

  Saturday, November 12, 2022

  AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUIPIGA 4-3 MTIBWA


  TIMU ya Azam FC imepanda kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa ugenini wa mabao 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani Morogoro.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo mawili dakika ya 18 na 30 na mabeki Abdallah Kheri dakika ya 41 na Daniel Amoah dakika ya 64, wakati ya Mtibwa Sugar yamefungwa na mshambuliaji Adam Adam mawili dakika ya 61 na 75 na kiungo Nassor Kiziwa dakika ya 76.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 23 katika mchezo wa 11 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi pointi tatu Yanga ambayo ina mechi tatu mkononi.
  Kwa upande wao Mtibwa Sugar wanabaki na pointi zao 15 za mechi 11 nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUIPIGA 4-3 MTIBWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top